Coastal Union
Mashindano

Wagosi wa Kaya kama Ulaya!

Sambaza....

Wanafainali ya AzamSports Federation Cup Coastal Union “Wagosi wa Kaya” wanafanya mambo yao kama timu za Ulaya tuu katika kuelekea fainali hiyo na msimu mpya wa Ligi Kuu.

Coastal Union imekua klabu ya kwanza kutambulisha jezi zao watakazotumia msimu ujao wa 2022/2023  utakoanza rasmi August 17 mwaka huu.

Jezi namba tatu “third kit” watakayotumia Coastal Union msimu wa 2022/2023.

Coastal imetambulisha jezi zake zote tatu za nyumbani, ugenini na jezi ya tatu ambazo watazitumia katika michuano yote msimu ujao wa Ligi.

Jezi ya ugenini watakayoitumia Coastal Union msimu ujao.

Wagosi wa Kaya “the mangush” kutoka Tanga wapinzani wa jadi wa Afrika Sports ni utamaduni wao kutumia rangi nyekundu na nyeupe.

Jezi ya nyumbami ya Coastal Union watakayoitumia msimu ujao wa 2022/2023.

Coastal Union ipo katika nafasi nzuri yakushiriki katika michuano ya Kimataifa msimu ujao. Endapo Coastal itaifunga Yanga katika fainali ya kombe la FA July 02 Arusha itakua imejikatika tiketi yakwenda kushiriki michuano ya kombe la shirikisho Afrika.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.