Shirikisho Afrika

Wapwa: Sina hakika kama mchumba huyu ni size ya muoaji au la!

Sambaza....

Muda mchache uliopita draw ya robo fainal ya kombe la shirikisho upande wa CAF imetoka na kujibu ‘kimuhemuhe’ cha washabiki wengi na wadau wa soka Tanzania kwamba Mnyama atapangwa na nani?

Pamoja na kuwa na timu nane kwenye hatua hii muhimu ya ngazi ya mtoano awali kulikuwa na mitizamo tofauti juu ya aina ya timu ambayo inapaswa kupangwa na Simba kati ya Al Ahli ,TP Mazembe na Orlando Pirates.

Kulikuwa na hoja tofauti huku chanya na hasi kwa pamoja, wapo waliokuwa wanaomba Simba ipangiwe timu nyepesi ( kama ipo) ili iwe rahisi kusonga mbele.

Sadio Kanoute akifunga bao mbele ya walinzi wa USGM

Wapo walikuwa wanasema hakuna timu nyepesi hapo angalau Mazembe kwa kuwa wanajuana ukanda  na Lunyasi apangiwe ngumu ili ajipime ubora wake na Msouth Africa huyu akitajwa kuwa kipimo

Mara baada ya draw kuchezwa na haya ndio majibu yake:

Simba SC 🇹🇿 | 🇿🇦 Orlando Pirates

Al Ittihad SC 🇱🇾 | 🇱🇾 Al Ahli Tripoli

Pyramids FC 🇪🇬 | 🇨🇩 TP Mazembe

Al Masry SC 🇪🇬 | 🇲🇦 RS Berkane

Swali ninalo jiuliza hapa Simba kama muoaji kapata ‘mke’ sahahihi wa kumuona au ndiyo hekaheka tupu ndoa ndoano?

Binafsi niwatowe shaka Orlando Pirates bado hawajajipambanunua vizuri katika ushiriki wake wa michuano ya CAF pamoja na ushiriki wao wa mara kwa mara.

Mwaka waliofanya vizuri ilikuwa 1996 kwenye ligi ya mabingwa na fainali ya kombe la shirikisho 2013 pamoja na 2015.Kifupi nao ni ‘washamba’ kama si wageni na njia naamini ni nafasi ya Simba kusonga mbele kama watakuwa na matumizi mazuri Estadio de Mkapa hiyo April 14.

Ushindi utakaoweka gape la goli tatu unaweza kukupa chochote kwa dhamana ya nusu fainali maana kuna ‘kitita’ cha maana zaidi.

Pale mwisho nimguse kipenzi cha Watanzania wengi Gabadinho Mhango aliwavutia alivyofunga goli katika AFCON akiwa na timu yake ya Malawi. Akifunga goli maridhawa la mbali akifanya vipimo vya kifizikia Force x Distance = workdone, sasa atakuja nchini akiwa’ hasimu’ wa mashabiki wake kwa maana ya kuwageuka basi miye nimwambie “Mgeni njoo mwenyeji apone.”

Sambaza....