Waziri Junior
Ligi Kuu

Wazir Junior asheherekea na Kandanda

Sambaza....

Mtandao wetu wa Kandanda.co.tz Leo hii umekabidhi zawadi kwa mchezaji aliyesajiliwa na klabu ya Yanga SC, Wazir Junior, ambaye aliibuka Galacha wa mabao kwa mwezi Juni-Julai wakati ligi ikimalika. Waziri Junior amefunga dirisha la zawadi zetu, baada ya kutoa jozi nane kwa wafungaji bora wa kila mwezi toka Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza.

Tuzo hizi zilikuwa zikidhaminiwa na Mgahawa Cafe & Restaurant ambao unapatikana mtaa wa Ohio katika jengo la Golden Jubilee Tower. Hakika umezifanya Tuzo hizi ziwe za kufana na kwa kuwafikia wachezaji wengi wa Ligi Kuu.

Wazir Junior, akipokea zawadi zake kutoka Mtandao wa Kandanda. Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Tovuti hii, Thomas Mselemu, akimkabidhi Wazir Junior.

Wazir Junior alikuwa mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Mbao FC iliyoshuka daraja msimu uliopita ambapo alimaliza msimu akiwa na magoli 14 nyuma ya mfungaji bora Meddie Kagere.

Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda akiwa na mshambuliaji wa Mbao fc Waziri JNR.

Klabu ya Yanga imemsajili Wazir Junior na rasmi msimu ujao atakuwa kwenye jezi ya njano na kijani. Akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz Wazir Junior ameahidi moto ule wa Mbao FC utaendelea akiwa Yanga.

“Kwanza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu ni kitu ambacho nilikuwa nakitamani kwa muda mrefu. Nilikuwa napigana ili siku moja nije kuchezea Yanga , nawaahidi mashabiki wa Yanga moto ule ule wa Mbao utaendelea nikiwa Yanga”- alisema Wazir Junior.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.