Mabingwa Afrika

Yanga ina Wachezaji wa Kawaida Ndani ya Timu Isiyo ya Kawaida

Sambaza....

Moja ya vitu ambavyo vilikuwa vinaonesha utofauti kati ya Yanga na Township Rollers katika mechi ya jana ni utulivu wa timu zote mbili.

Utulivu ambao ulifanya kutengeneza mstari wa utofauti wa utengenezaji na matumizi ya nafasi.

Township Rollers hawakuwa na presha kubwa ndani yao, kitu ambacho kiliwafanya wawe watulivu na kufanya maamuzi ya uhakika ndani ya timu.

Maamuzi ambayo yalienda sambamba na ushirikiano wa timu kwa ujumla. Timu ilipokuwa inaenda kushambulia, wachezaji wote walionekana kushirikiana kwenda kushambulia na timu ilipokuwa inashambuliwa wachezaji wote walishirikiana kukaba kwa pamoja na kwa nidhamu.

Nidhamu ambayo iliwafanya wajijenge vizuri na kuonekana bora kwa ƙkila kitu walichokuwa wanakifanya ndani ya uwanja.

Ukamilifu wa timu unaletwa na wachezaji kamilifu kwenye kila idara, Township Rollers walikuwa wakamilifu kwenye mechi ya jana.

Image result for yanga vs township rollers images

Hii ilikuwa tofauti sana na kwa upande wa Yanga, mfano eneo la katikati la Yanga ambalo lilikuwa na Pato Ngonyani na Papy Kabamba lilikuwa na ushirikiano hafifu.

Kwanini nasema hivo? Pato Ngonyani alionekana na msaada mkubwa sana kipindi ambacho timu ilikuwa inakaba, lakini timu ilipokuwa inataka kushambulia msaada wake haikuwa mkubwa sana kwa sababu Pato Ngonyani hakuwa anaisukuma timu kwenda mbele.

Hali ambayo ilikuwa inamlazimu Papy Kabamba kuwa na jukumu yeye kama yeye bila msaada wowote, majukumu yalikuwa mengi kwake tena dhidi ya wachezaji ambao walikuwa wamekamilika.

Kitu hiki kiliwasababisha kina Emmanuel Martin na Pius Buswita kutopata mipira mingi.

Hata wakati ambao kina Emmanuel Martin , Pius Buswita, Ibrahim Ajib walipokuwa wanahitajika kusaidia kuchukua mipira katikati hawakuwa na uwezo, hali ambayo iliwafanya wapwaye kwa kiasi kikubwa.

Image result for yanga vs township rollers images

Hakukuwepo na mchezaji ambaye angeweza kuibeba timu kwenye wakati huo mgumu kwa sababu Yanga ilikuwa imejaza wachezaji wa kawaida kwenye timu isiyo ya kawaida ndiyo maana wanapata matokeo ya kawaida.

Hata kwenye benchi hakukuwepo na mchezaji ambaye angeweza kuingia na kubadilisha hali ya mchezo ndani ya mchezo.

Kwenye mashindano haya ya kimataifa unatakiwa uwe na wachezaji wa hadhi ya michuano hii ili timu ifike mbali.

Ni ngumu kupata matokeo makubwa kama unawachezaji wengi wa kawaida ndani ya timu yako.

Yanga walipofika robo fainali ya kombe la shirikisho misimu miwili iliyopita, ilikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo dakika yoyote

Kipindi hiki Yanga haina tena wachezaji hao kwenye kikosi hiki, wana wachezaji wengi sana wa kawaida ndani ya kikosi chao

Ni kitu ambacho wanatakiwa kujifunza zaidi, wanapozidi kupata nafasi ya uwakilishi wa kimataifa, wanatakiwa kupata wachezaji ambao wana hadhi ya mashindano husika.

Huwezi kufika mbali kama unaidadi kubwa ya wachezaji ambao hawajajengeka kwa kiasi kikubwa.

Ni jambo jema kuwaona kina Ramadhani Kabwili kuwaona wakianza kwenye michuano mikubwa kama hii, lakini wachezaji hawa vijana wanatakiwa wazungukwe na wachezaki wa madaraja ya juu ili wawe na uwezo wa kujengeka na kuimarika katika misingi ya ushindi ndani yao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x