Stori

Yanga katika tumaini jipya la usajili? – 1

Sambaza....

Binafsi niliyoyaona kwenye kilele cha sherehe za wiki ya mwananchi sipendi sana kwenda kwenye vitu vya nje ya mchezo juu ya mpangilio wa shughuli nzima .

Nitumie mstari moja tu kupongeza kundi la sarakasi, lile ndio lililoninogea zaidi utundu wa wale madogo wanaocheza na baiskeli kwangu walinipa burudani kubwa sana,katika vitu usivyovifahamu toka kwangu Mimi ni mpenzi sana wa sarakasi.

Tukiangalia game yenyewe ,actual ilikuwa na mvuto mzuri kwa sababu ya resistance ya pande mbili ,ndio maana pamoja na red card kutolewa bado battle lilikuwa heavy kana kwamba hakuna timu moja inacheza pungufu.

Kiu kubwa kuwaona wachezaji wapya wa Yanga wa ndani na wa nje kwa maana ya Mataifa wanaotoka lakini kabla sijaenda mbali niseme Fei Toto ndio alikuwa mwenye game yake, awali niliwahi andika juu ya Fei Mara mbili tatu, ila kuna siku tutaelewana lugha Ile ilikuwa super performance.

Shomari kibwana na Yasini Mustapha walikuwa na ladha zao, hasa Mustapha ambaye sikumuona kupoteza mpira hata moja ,alikuwa na matendo sahihi kwa zaidi ya 95%.

Mwamnyeto na Ninja waliwajibika vizuri kwa mawasiliano makubwa ,walijiamini hadi kuna muda wakapitiliza Mwamnyeto alianza kufanya kazi za viungo kwenye kuwapiga kanzu washambuliaji nimkumbushe ni risk sana hasa kwa nature ya timu yake hiyo mpya!

Mukoko Tonombe

Mukoko ,Tuisila Sarpong na Carlinhos
Namatumini ndio walikuwa na mvuto zaidi kwa watazamaji kabla na ndani ya mchezo.

Mukoko Tunombe hakuanza vizuri katika dk 15 za mchezo hope ni atmosphere au kupania kuonesha makubwa lakini kadri muda ulivyokuwa unakwenda aka adopt mazingira akaanza kuitendea haki wizara yake ya kiungo wa ulinzi kifupi alicheza vyema

Tuisila type ya akina Cr7 dribbling imejengwa na too much feint hata sehemu isiyohitaji feint  (nakshi) lakini pamoja na yote anakumbuka kucheza kwa faida ya timu ni winga wa kushoto kwa Jana walivyompanga lakini matumizi ya mguu wa kushoto yapo chini,silaha yake kudumbukia ndani ili aweze kupasia au kupiga far post kwa mtindo wa curve.

Unawezaka kumuona katika goli alilofunga alifanya touch moja huku akishape body yake ili kuucurve.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.