Viongozi wa Yanga na GSM katika hafla ya utiaji saini ya uhusiano na Laligaga
Blog

Yanga kujenga uwanja Kigamboni

Sambaza....

Baada ya kumalizika vyema kwa tamasha la wiki ya mwanachi, mipango yote imeelekezwa kwenye ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa Yanga.

Injinia Hersi amezungumzia suala hilo na kudhibitisha kuwa ujenzi as uwanja wa mazoezi ya Yanga utaanza hivi karibuni.

Viongozi wa Yanga

“Ule uwanja ambao tulipewa na mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa wakati huo Paul Makonda tumeanza kufanya design na kutafuta mtu wa kufanya naye kazi”.

“Na tumepanga kuwa na viwanja viwili vya mazoezi. Kiwanja cha nyasi bandia na kiwanja cha nyasi ya kawaida pamoja na GYM. Kwa hiyo tuko hatua ya mwisho ya kutafuta mtu wa kufanya naye kazi na hivi punde kamati ya miundombinu kupitia mwenyekiti wake Injia Mwaseba watakuja na taarifa rasmi”. Alimalizia Injinia Hersi


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.