Ligi Kuu

Yanga kuvaa nembo nyeusi ya Vodacom

Sambaza....

Baada ya klabu ya Yanga kutoa tamko hii leo kuhusiana na suala la rangi ndani ya klabu hiyo kuwianisha na mdhamini. Meneja wa Masoko wa TFF,  Aaron Nyanda, amesema kwamba klabu ya Yanga itaendelea kuvaa logo yenye rangi nyeusi kama ilivyokuwa hapo awali.

Jezi za Yanga wakati Vodacom ikiwa ni mdhamini wa Ligi Kuu (Maktaba)

Nyanda amesema kwamba anaushangaa uongozi wa Yanga kuanza kulalama kupitia vyombo vya habari bila kupata taarifa rasmi ya shirikisho.

Nyanda ameongeza kwamba uongozi wa Yanga ulipaswa kuwasiliana na Tff juu ya jambo hilo kwani wao ndio wahusika kamili wa swala hilo.

Vodacom alipokuwa akitangazwa mdhamini wa Ligi Kuu kuanzia msimu wa 2019/20

Lakini pia ameiasa klabu hiyo kuwa sasa inapaswa kuweka mikakati yao kwenye mchezo wao wa kimataifa na kuendelea kuiunga mkono timu ya Taifa katika mchezo wa kusaka tiketi ya kuingia katika makundi ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.