Abdalah Shaibu "Ninja"
CECAFA

Yanga nayo yaikimbia As Vita, yajitoa Kagame

Sambaza kwa marafiki....

Juzi Simba Sc ilitoa taarifa ya kujiondoa katika mashindano ya klabu bingwa Afrika mashariki na Kati (Kagame Cup). Leo hii imetoka barua ya Yanga kujitoa katika mashindano hayo.

Yanga imetoa sababu nyingi za wao kujitoa katika mashindano hayo ambayo yanatarijiwa kuanza mwezi wa 7 mwaka huu, sababu ambazo zimeifanya Yanga kujitoa ni zifuatazo.

-Wachezaji wengi wa Yanga kumaliza mikataba yao.
-Wachezaji ambao Yanga wamepanga kuwasili msimu huu bado hawajakamilisha taratibu za kujiunga na Yanga.
-Baadhi ya wachezaji na makocha watakuwa kwenye michuano ya Afcon nchini Misri.
-Wachezaji wachache wenye mikataba wameshapewa ruhusa ya mapumzuko ya mwisho wa ligi.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.