Stori

Yanga: Tutamlinda Musonda

Sambaza....

Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa maoni yao wakati mshambuliaji wao Kenedy Musonda akikabidhiwa zawadi ya medali kutoka nchini Hispania.

Musonda alikabidhiwa medali ya zawadi kutoka kwa mtoto Lucas Gomez raia wa Hispania aliyewakilishwa na balozi wa Hispania nchini George Molagas. Zawadi hiyo Musonda ameipata kutokana na kucheza vyema alipokua Power Dynamos.

 

Akizungumzia tuzo hiyo msemaji wa klabu ya Yanga wamesema wanafurahia kwa alichofanya Musonda lakini pia watafanya kazi kubwa kumzuia maana tayari amejiweka sokoni.

“Tumefurahishwa na hiki ambacho kimefanywa kwa mchezaji wetu kwa sababu kitamuongezea thamani mchezaji huyo na ari ya kupambana.

Kubwa sasa inatakiwa tuwe macho kuona tunamlindaje mchezaji wetu kwa sababu kwa hiki bila shaka macho ya watu wengi yatakuwa kwake zaidi. Lakini ni faraja kwa upande mwingine kuona mchezaji anapata ‘connection’ kubwa.” Alli Kamwe

Sambaza....