Beno Kakolanya
Ligi Kuu

Yanga yaachana rasmi na Beno Kakolanya

Sambaza kwa marafiki....

Kwa muda mrefu kumekuwepo na Sintofahamu kati ya Yanga na aliyekuwa golikipa wao namba moja Beno Kakolanya.

Sintofahamu hiyo ilianza baada ya Beno Kakolanya kugoma kushinikiza madai ambayo alikuwa anawadai Yanga kutokana na kutolipwa pesa yake ya usajili.

Mgomo huo ulionekana kuithari timu hivo kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alikataa kuendelea kuwa na mchezaji ambaye hajitolei kwenye timu hivo akaamua kutomtaka Beno Kakolanya katika timu yake.

Kimepita kipindi kirefu tangu Beno Kakolanya akiwa nje ya timu ya Yanga. Mtandao huu uliamua kufuatilia kipi kinachoendelea kwenye sakata hili.

Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Bwana Kaaya amedai kuwa suala la Beno la Yanga limeshamalizika muda hadi wao wameshalisahau.

“Hili suala limemalizika muda, na tumeshalisahau kabisa, Beno Kakolanya siyo mchezaji wa Yanga mpaka sasa hivo”. Alisema kaimu katibu mkuu huyo wa Yanga.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.