Blog

Zahera hana huruma, apania kuwafilisi YANGA

Sambaza....

Muda kadhaa umepita mpaka sasa hivi tangu Yanga ilipoamua kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera kutokana na timu kutofanya vizuri katika michezo ya kimataifa Baada ya kutolewa na Pyramid FC ya Misri.

Baada ya kuachana na Yanga Mwinyi Zahera alikuwa bado anawadai Yanga haki zake na mpaka kufikia muda huu Yanga hawajafanikiwa kumlipa , pamoja na hali Mbaya ya kiuchumi ya Yanga kocha huyo amepania kula nao sahani moja ili wamlipe pesa zake.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amethibitisha kuwa ameishtaki klabu ya Yanga katika shirikisho la soka duniani (FIFA) kuhusu madai yake. Zahera amedai Klabu ya Yanga itamlipa mara mbili ya madai yake na gharama za kufuatilia madai yake.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.