Sambaza....

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, ameachana na klabu hiyo siku tano baada ya kuipa taji la tatu mfululizo la klabu bingwa Ulaya.

Zidane alitangaza uamuzi huo siku ya Alhamisi mbele ya rais wa klabu hiyo, Florentino Pérez.

Nimechukua huu umuzi wa kutokuendelea msimu ujao. Kwangu mimi na kwa kila mtu, nadhani ni wakati wa mabadiliko umewajia. Haukuwa uamuzi rahisi kwangu” Amenukuliwa wakati akitangaza uamuzi huu.

Rekodi ya Zinedine Zidane kama kocha wa Real Madrid:


Michezo 149
Mabao 393
Kushinda 104
Sare 29
Kupoteza 16
Makombe 9

Uchambuzi kamili wake utafuata….

Sambaza....