Abdul Hillary (KMC FC)
Ligi Kuu

Abdul Hillary aongezewa ‘Mguu”.

Sambaza....

Wakati gani unahitaji kusheherekea? bila shaka ni wakati ambapo umefikia malengo ya kipindi husika. Hii ndio maana wachezaji hadi makocha hushangilia kwa ku’slide’, ikionyesha jinsi raha ilivyo katika kupachika bao.

Kandanda ikishirikiakiana na Mgahawa Cafe, huchukua shangwe ile uwanjani kila mwezi na kuileta nje ya uwanja kwa kusheherekea na mchezaji ambaye alifunga mabao mengi katika Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya mwezi husika.

Mdau wa Kandanda, Gerald akimkabidhi Hillary kiatu kwa niaba ya Kandanda.

Leo tumemkabidhi zawadi zake Abdul Hillary, mchezaji wa KMC baada ya kuibuka galacha wa magoli wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa mwezi Disemba 2019.

Kwa upande wake ameishukuru Kandanda kwa kutambua juhudi zake uwanjani na kukiri hii itawaongezea motisha wachezaji wengi ili kufunga zaidi.

Kiatu alichopewa Abdul Hillary kina jina lake kabisa

Abdul Hillary akiwa na zawadi zake kutoka Kandanda

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.