Jana mtandao wa kandanda. co.tz ulifanikiwa kumpa zawadi ya kiatu Abdul Hillary ambaye ni mchezaji wa KMC baada ya kuibuka mfungaji bora wa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana.
Wakati gani unahitaji kusheherekea? bila shaka ni wakati ambapo umefikia malengo ya kipindi husika. Hii ndio maana wachezaji hadi makocha hushangilia kwa ku'slide', ikionyesha jinsi raha ilivyo katika kupachika bao.