Sambaza....

Uongozi wa klabu ya soka ya AFC Leopards umetuma malalamiko yake kwa mamlaka husika ikiwemo shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu Simba SC kumtumia beki Lamine Moro wakati ni mchezaji halali wa Buildcon FC ya Zambia.

Hiyo ni baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Simba katika mchezo wa michuano ya SportPesa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lamine Moro aliyepiga mpira mbele ya mkude

Saul Shikuku ni mjumbe kamati utendaji ya klabu ya soka ya AFC Leopards na hapa anaelezea malalamiko yake mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Sauti ya Saul Shikuku, Mjumbe kamati Tendaji AFC Leopards

Mabao ya Simba katika mchezo huo yamepatikana kupitia kwa Emmanuel Okwi na Cletous Chama, na sasa Simba wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali na Bandari FC waliowatoa Singida United.

Sambaza....