Blog

African Lyon kubadilisha Gia mechi ya Yanga.

Sambaza....

Meneja wa klabu ya Soka ya African Lyon ya Jijini Dar Es Salaam Adam Kipatacho amesema mechi tatu za Mwanzo wa Ligi Walizocheza Kanda ya Ziwa zimewapa maono ya Namna Ligi Ilivyo Kwa Sasa.

Kipatacho ameuambia mtandao wa kandanda.co.tz kuwa funzo ambalo wamelipata katika michezo hiyo litawasaidia kujua kitu gani wakifanye katika mechi zijazo ili ile tabia ya kushuka na kupanda ligi ikome na kuwa kudumu kwa muda mrefu zaidi.

“Kusema ukweli tumejifunza mambo mengi sana, japokuwa African Lyon imekuwa inapanda na kushuka na tulisema muda huu hatutegemei kutokea yale yaliyotokea, mechi yetu ya kwanza tulipoteza dhidi ya Stand, tukatoka sare na Alliance na Kagera, kusema ukweli tumejifunza mengi sana,”

“Mwalimu ameona matatizo yaliyojitokeza, nafikiri ndo maana umeona sasa hivi tunafanya mazoezi magumu sana kuelekea katika mechi yetu ya Yanga lakini pia mechi ya ligi dhidi ya Coastal Union,” Kipatacho amesema.

Aidha kuelekea katika mchezo wao wa kirafiki dhidi Yanga Jumapili ya wiki hii, Kipatacho amesema mwalimu atautumia mchezo kujaribu aina nyingine ya uchezaji ambayo ni ushambuliaji ili watakapocheza na Coastal Union waweze kufunga mabao mengi zaidi.

“Mwalimu amekuja na Plan nyingine, jinsi gani ya kupata ushindi nyumbani kwa sababu away tulikuwa tunacheza formation nyingine jinsi gani ya kujilinda,  lakini sasa hivi tunataka kushambulia ili tuweze kupata ushindi,” ameeleza.

Wachezaji wa African Lyon walipewa likizo ya siku moja na waliripoti Jumanne kuanza mazoezi upya katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga na baadae dhidi ya Coastal Union.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x