
Imeripotiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, amekamatwa na mamlaka nchini Ufaransa alikokuwa akihudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).
Taarifa hizi zimethibitishwa na FIFA, lakini hakuna sababu za wazi za kukamatwa kwake zaidi ya kusema zinahusiana na mamlake yake akiwa rais wa CAF. Fifa haifahamu kwa undani kuhusu uchunguzi au tuhuma hizo ndio maana haijatoa taarifa kamili.

Ahmad Ahmad anahusishwa na mkataba wa CAF na Puma, kampuni ya vifaa vya michezo.
Hivi karibuni pia kulikuwa na tuhuma ambazo katibu mkuu wa CAF aliziwasilisha FIFA zikitaja tuhuma za rushwa za Ahmad Ahmad na malipo kwenda kwa marais wa mashirikisho.
Unaweza soma hizi pia..
Waandishi wa habari za michezo waigalagaza Unitalent.
Unitalent hawakuishia tuu kufungwa mabao mawili lakini pia waliteseka uwanjani haswa katika eneo la kiungo
Mechi Iliyoamua mshindi hatua ya Makundi Kombe la Dunia
Hii ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 1950, mechi ya Uruguay dhidi ya Brazil. Mechi ambayo iliamua mshindi hatua ya makundi.
Kwanini Boban Hakuyapenda Maisha Ya Ulaya…?
Yumkini Haruna Moshi alishawishiwa kutokukipenda ambacho kingemsaidia maishani. Soma stori hii
Chama cha Soka Afrika Kusini waishtaki Simba CAF.
Na ina uwezo wa kuharibu uwanja na tunaamini haikuwa kwa njia yoyote inayohusiana na michezo