ASFC

Ajib afunga goli lake la kwanza, Chama afufuka!

Sambaza....

Baada ya Jana kushuhudia Yanga wakishinda goli 4-0 dhidi ya Iringa United kwenye uwanja wa Uhuru , leo hii tumeshuhudia Simba katika kipindi cha kwanza wakienda huku wakiwa wanaongoza kwa goli 4-0.

Magoli manne (4) ya Yanga yalipatikana katika kwenye vipindi vyote , ila mpaka muda huu wa mapumziko Simba imeshafunga magoli 4 kwenye kipindi hiki cha kwanza.

Magoli ya Simba yamefungwa na Chama likiwa goli lake la kwanza la mashindano na goli ambalo linaonesha urejeo wake Baada ya kuonekana kushuka kiwango msimu huu.

Magoli mengine yamefungwa na Deo Kanda likiwa goli lake la pili la kimashindano msimu huu , Gerson Fraga amefunga goli kwenye hii mechi huku Ibrahim Ajib akifungua ukurasa wa magoli kwenye mechi za mashindano akifunga goli lake la kwanza la kimashindano.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.