Ligi Kuu

Alli Kamwe: Yanga imeifunga Yanga B!

Sambaza....

Anaandika Alli Kamwe:
Mambo 10 nilioyaona Dodoma Jiji vs Yanga

1: WHAT A WIN  POINTI 3 MUHIMU KATIKATI YA PRESHA KUBWA. WELL DONE WANANCHI  Vile ndio timu yenye dhamira ya Ubingwa inatakiwa kurejea baada ya nyakati ngumu

2: ILE ‘PITCH’ ya Jamhuri ni AIBU! ‘Standard’ ya Game inapotea kwa pitch kukosa viwango. Nawaza, Rais Samia alipotoa agizo la VIWANJA ni watu hawakuelewa au ni kusudi tu? Kuna jambo la haraka inabidi kufanyika pale

3: ‘FIGHTING SPIRIT’ ya wachezaji wa Yanga ilitosha kueleza kilichokuwa kwenye vichwa vyao. Walikimbia kilomita nyingi sana.. walipambana kushinda ‘Second Balls’ nyingi! Kubwa zaidi walilobadili leo, YANGA KWANZA, MAYELE BAADAE.

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele akizibitiwa na mlinzi wa Dodoma Jiji Mgalula.

4: ‘Tactically’ Kocha wa Dodoma Jiji ni kama alijiandaa kudili na Ufundi wa Yanga katikati ya uwanja Lakini bahati mbaya kwake, Yanga wakaja tofauti? Kivipi?

5: Nabi akarusha karata tofauti. Kutokana na changamoto ya Pitch, akaweka wachezaji sahihi katika kiwanja kile. Akaiacha akili ya Bangala na Aucho akaja na mpango wa kutegemea mapafu ya kina Mauya na Ambundo

6: Yanga wakaupeleka mchezo pembeni kwa kasi kubwa. Moloko na Ambundo wakawa kwenye kiwango chao bora. Mauya akawa Form pia kwenye kuutembeza mpira kwa kasi. Kuna jambo Yanga wamejifunza pia kwenye lile bao la kwanza! Lipi?

Dickson Ambundo akimuacha mlinzi wa Dodoma Jiji.

7: Pasi ya Moloko kwenda kwa Ambundo ni matokeo ya Yanga kujua faida ya kutumia Movement za Mayele uwanjani. Huwezi kuzuia Mabeki kumkamia Mayele lakini unaweza kuwaadhibu kiufundi kwa mikimbio ya kutokea pembeni

8: Emmanuel Martin.. Mchezaji wa mechi kutoka kikosi cha Dodoma Jiji.. Alivyorudi kucheza chini ni kama uimara wake ukaongezeka. Akawa mzuri kwrnyr kukaba na kushambulia

9: Diarra  WHAT A PERFOMANCE. SAVE MBILI BORA SANA ZA MECHI. Ziko nyakati ubora wa kipa unaweza kuisaidia Timu kushinda mechi kwa kufanya Saves za kukata presha ya wapinzani

Zawadi Mauya na Fiston Mayele wakishangilia goli la pili

10: Bao la 2 la Yanga ni OFFSIDE. Kama Shuti la Mauya lingekwenda moja kwa moja, hakuna tatizo. lakini kipa kuucheza, tunarudi kutazama kuangalia nafasi ya Ambundo na Mayele wakati Mauya anapiga mpira. Walikuwa eneo la kuotea na waliuingia mchezo! Sijaelewa kwanini FRANK KOMBA alinyoosha na kushusha kibendera kwenye Tukio lile

Nb: ‘YANGA A’  2-0 ‘YANGA B’ 

Sambaza....