Ligi Kuu

Alliance FC ‘kuanza ligi’ dhidi ya African Lyon.

Sambaza....

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Soka ya Alliance ya Jijini Mwanza Jackson Luka Mwafulango amesema maandalizi kuelekea katika mchezo wa pili wa ligi dhidi ya African Lyon yanaendelea vizuri.

Mwafulango amesema kwa sasa wamesahau yaliyopita katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mbao ambapo walipoteza kwa bao 1-0, na wanajipanga kuhakikisha hawafanyi Makosa Mengi katika mchezo ujao ili kuweza kuibuka na ushindi.

“Tunafahamu wenzetu watakuwa na mbinu nyingine tofauti na yetu, wakiwa wanafahamu kuwa nao wamepoteza mchezo uliopita, lakini sisi chini ya kocha Mbwana Makata kikosi kimeendelea na mazoezi kurekebisha makosa ya mchezo uliopita,” Mwafulango amesema.

Amesema maandalizi yanaendelea vizuri na tayari wameanza mazoezi kuelekea katika mchezo huo ambao utafanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza siku ya Jumatatu.

Mechi za Leo Jumamosi:


Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x