Ligi Kuu

Alliance wajichimbia Iringa kuwawinda Mbeya City.

Sambaza....

Timu ya soka ya Alliance imeendelea na maandalizi ya mchezo wake ujao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumapili ya Septemba 16, 2018 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Taarifa ya klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema kuwa mchezo huo ni mchezo muhimu kwao kwani utakuwa ni mchezo wa nne (4) wakicheza tangu kuanza kwa ligi huku

wakifanikiwa kupata sare katika mchezo mmoja dhidi ya African Lyon, kufungwa michezo dhidi ya Mbao FC na Tanzania Prison.

“Tunafahamu kuwa na wenyeji wetu kwao utakuwa ni mchezo wa nne kama sisi na wakiwa hawana point yoyote baada ya kufungwa michezo yote mitatu waliyoicheza huko nyuma na wataingia kwania yakutaka kupata point  ili kujiweka sawa katika ligi hasa ukizingatia kuwa mchezo huo utakuwa ndiyo wa kwanza kwao kucheza nyumbani kwani michezo yote mitatu ya mwanzo walikuwa ugenini” imesema taarifa hiyo.

“Pamoja na yote hayo timu yetu inaendelea na mazoezi huku  mkoani Iringa  kwa umakini mkubwa na kambi yenye kila aina ya hamasa kuelekea mchezo huo kwani hadi sasa hakuna majeruhi yeyote yule ambaye anaweza kuwa kwenye hatihati ya kuukosa mchezo huo kwani vijana wote wapo vizuri na kila mmoja wetu kwenye timu anaonesha hamu ya kutaka kucheza mchezo huo” Imeongeza.

Kwa mujibu wa afisa habari wa Alliance Jackson Luka Mwafulango amesema wataingia uwanjani wakiwa wanaiheshimu timu ya Mbeya City kutokana na ubora wao na uzoefu wao katika ligi kuu na kwamba hawataingia kichwa kichwa kutokana na matokeo waliyo yapata huko nyuma kwani wanaamini hayo nisehemu ya mchezo na wao wanajipanga vizuri kukabiliana nao.

“Mwisho naendelea kuwaomba mashabiki na wadau wa soka hasa wanao ipenda timu yetu waendelee kutuunga mkono na kutuombea kamwe wasikate tamaa na kutuacha kwani katika mpira kuna wakati utalia sana, utacheka sana na utahuzunika sana kwahiyo sisi kama timu tunaitafuta dawa ya wao kucheka sana kwa kukiandaa kikosi vizuri na umakini mkubwa na tunaamini siku siyo nyingi watacheka na kutamba kisawasawa,” imesema.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x