Ligi Kuu

Azam kujimaliza yenyewe mbele ya Simba!

Sambaza....

Leo kutakua na mchezo mwingine na Ligi Kuu ya NBC ambapo Azam Fc watakua wenyeji wa Simba katika Uwanja wao wa Azam Complex Chamanzi nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.

Katika mchezo wa duru la kwanza Azam walikubali kipigo cha mabao mawili kwa moja katika dimba la Benjamin Mkapa. Goli la Azam lilifungwa na Rodgers Kola wakati yale ya Simba yalifungwa na Osmane Sakho na Sadio Kanoute.

Kiungo wa Simba Rally Bwalya akiwatoka walinzi wa Azam Fc.

Kuelekea mchezo huu utakaopigwa Chamanzi ni wazi Simba ana kila sababu ya kupata matokeo mbele ya Azam Fc kutokana na sababu nyingi za kiufundi.

Mtazame hapa Tigana Lukinja akiuchambua ubora wa Simba utakaoipa matokeo mbele ya Azam Fc ugenini Chamanzi.


Sambaza....