Chupa ya zawadi kwaajili ya Makambo, ambayo tovuti ya kandanda hutoa kwa wachezaji kila mwezi.
Ligi Kuu

Baada ya Molinga na Bocco kutupia tazama vita ya ufungaji bora ilivyonoga!

Sambaza....

Michezo  mitano  ilipigwa jana katika viwanja mbalimbali nchini katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara huku mshambuliaji wa Biashara United akiingia katika vitabu vya rekodi msimu huu.

Atupele Green anakua mchezaji wa sita kuweza kufunga mabao matatu “hatrick” msimu huu badaa ya jana kuiwezesha timu yake Biashara Utd kuibuka  na ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya KMC.

Katika mchezo uliopigwa jijini Mbeya Papaa John Bocco “Adebayor” amezidi kunogesha sherehe za ubingwa kwa Mnyama baada ya kufunga mabao mawili mbele ya wagonga nyundo Mbeya city na kuipa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri Simba.

John Bocco akiifungia Simba bao mbele ya Aroon Kalambo wa Mbeya city.

Lakini pia Papaa Molinga nae hakua nyuma baada ya kuweka kambani bao mbili mbele ya Namungo fc na hivyo kuisaidia Yanga isipoteze mchezo baada ya mapema tuu Edward Manyama kuipa uongozi wa mabao mawili Namungo fc.

David Molinga “Falcao”

Yusuph Mhilu wa Kagera nae ameendeleza moto wa kufunga mabao msimu huu baada ya kuifungia bai moja timu yake na kuipa ushindi mwembamba mbele ya Azam fc katika dimba la Kaitaba.

Yusuph Mhilu akishangilia baada ya kufunga goli lake katika mchezo dhidi ya Azam fc.

 

Tazama hapa chati ya ufungaji wa mabao baada ya magoli ya jana.

Galacha wa mabao

Na.MchezajiTimuNafasi
1tanDaniel Richard MaranyaKiungo0
2tanEzekia MwashilindiMshambuliaji1
3rwaPatrick SibomanaMshambuliaji6
4tanOmary MpondaMshambuliaji1
5tanBakar N. MwamnyetoMlinzi0
6tanEdward Joseph SongoKiungo4
7Elinyesia SumbiMshambuliaji2
8tanAlly Nassor UfuduKiungo0
9tanAtupele Jackson0
10tanEdward Charles0

Sambaza....