Aliekua Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji.
Ligi KuuTetesi

Baada ya tishio la BMT, Manji kurejea rasmi Yanga

Sambaza....

Baada ya jana Baraza la michezo Tanzania (BMT) Kuitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi kuziba nafasi za viongozi ambao walijiudhulu na kuacha nafasi hizo wazi, kuna taarifa ya kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji anatarajia kurejea rasmi katika klabu hiyo.

Yusuph Manji ambaye aliandika barua ya kujiudhulu Uenyekiti wa klabu ya Yanga baada ya kuonekana kukumbwa na matatizo binafsi ambayo yalimfanya asimudu kufanya vyema majukumu ya klabu ya hiyo.

Taarifa za ndani zinasema kuwa Yusuf Manji atarejea katika nafasi yake ya Uenyekiti. Hivo Uchaguzi utafanyika kuchagua nafasi zingine.

BMT imeliagiza shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF), kusimamia uchaguzi huo wa Yanga kuziba nafasi ambazo zimeachwa wazi baada ya viongozi mbalimbali wa Yanga kujiudhulu.

Viongozi ambao walijiudhulu nafasi zao ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji, Mwenyekiti msaidizi wa klabu hiyo Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo ya Yanga. Ambapo mpaka sasa kuna wajumbe sita (6) kati ya wajumbe 13 wanaotakiwa kikatiba. Hii inafanya kamati tendaji kutofanya maamuzi yake vizuri kwa mujibu wa katiba.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x