Benno akiwa Yanga
Blog

Benno Kakolanya na majuto ya Dodoma na milioni 10.

Sambaza kwa marafiki....

Kipa wa zamani wa Tanzania Prisons na timu ya Taifa Benno Kakolanya huenda akawa kwenye majuto ya hali ya juu kutokana na mgogoro wake dhidi ya klabu yake ya Yanga sc.

Kutokana na kuhitilafiana na Yanga katika masuala ya kimkataba ilipelekea Benno kujiweka pembeni katika klabu yake ya Yanga na kugoma kuendelea kuichezea klabu hiyo mpaka pale atakapolipwa stahiki zake.

Kutokana na kugoma kuichezea Yanga Benno amepoteza nafasi yake ya kua kipa namba mbili nyuma ya Aishi Manula Stars chini ya Amunike na nafasi yake kuchukuliwa na Menata Mchata kutoka Mbao fc.

Walinda lango wa Stars wakipokea maelekezo katika mazoezi ya timu ya Taifa.

Benno Kakolanya mpaka sasa amekosa kiwanja Dodoma pesa taslim milioni kumi na pia ni dhahiri shahiri atakosa nafasi ya kua katika kikosi kitakachoshiriki Afcon nchini Misri mwaka huu.

Kakolanya atakua katika majuto makubwa kwake na familia yake kwa kuigomea Yanga akishinikiza apewe stahiki zake lakini akikosa nafasi adimu na kuandika historia ya kushiriki michuano mikubwa kabisa barani Africa.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.