Ligi Kuu

Bila Morrison na Molinga Yanga ingekuwa inashika nafasi ya 13 !

Sambaza....

Jana Bernard Morrison aliinusuru timu yake ya Yanga kutofungwa na Mbeya City katika mchezo ambao ulifanyika katika siku ya kuzaliwa kwao wakiwa wanasherehekea miaka 85 tangu timu ianzishwe.

Bernard Morrison tangu atue katika kikosi cha Yanga amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Yanga ambapo mpaka sasa hivi kwenye ligi kuu Tanzania bara amefanikiwa kucheza mechi 6 akiwa na Yanga huku akifunga magoli 3 na kutoa pasi 2 za magoli.

Jana ameisaidia Yanga kupata alama moja , na mpaka sasa hivi amesaidia Yanga kupata alama 8 za moja kwa moja. Mfano jana kwenye mechi dhidi ya Mbeya City iliyoisha kwa sare ya 1-1 point hii aliileta moja kwa moja yeye.

Mechi dhidi ya Lipuli ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda 2-1 , Bernard Morrison alifunga goli , kama ukitoa goli lake Yanga ingetoka sare Lakini goli lake ambalo ndilo lilikuwa goli la pili la Yanga , goli la maamuzi ya kuchukua alama tatu liliipa Yanga alama 3 . Hivo jumla ya alama 4 hizo zinakuwa .

Mechi ya Yanga na Tanzania Prisons ambayo Yanga walishinda magoli 2-0 , Bernard Morrison alifunga goli moja na kutoa pasi ya mwisho ya goli , hivo kuhusika kwenye alama zote tatu za mchezo huu hivi kufikisha alama 7 ambazo ameipa Yanga katika michezo 6 aliyocheza.

Kwenye michezo hiyo 6 Yanga imepata alama 16 huku alama 7 na alama 6 zimetoka kwa Molinga ambaye aliwapa Yanga moja kwa moja alama 6 kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar alipofunga goli pekee la ushindi na mechi dhidi ya Ruvu shooting .

Kwa hiyo David Molinga na Bernard Morrison katika michezo 6 iliyopita , michezo ambayo ndiyo aliyocheza Bernard Morrison tangu afike Yanga wameipa Yanga alama 13 za moja kwa moja Kati ya alama 16 walizopata Yanga.

Kwa hiyo ukichukua alama 38 walizonazo Yanga ukitoa na alama 13 zilizopatikana moja kwa moja kutoka kwa David Molinga pamoja na Bernard Morrison, Yanga ingekuwa inashika nafasi ya 13 mbele ya Alliance FC kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa huku wakiwa wanalingana alama 25.

Mechi ambazo Bernard Morrison amecheza akiwa na Yanga ni Singida 1-3Yanga , Yanga 2- 0Tanzania Prisons, Yanga 1- 0 Mtibwa , Yanga 2-1 Lipuli FC , Ruvu Shooting 0- 1 Yanga na Yanga 1-1 Mbeya City.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.