Sambaza....

Katibu wa matawi ya klabu ya Yanga, Bwana Boaz Ikupilika amewaasa Wanayanga kuongeza kasi ya uchangiaji ili kuipa hamasa timu yao kushinda mchezo wa jumapili.

Huu ndio ujumbe to uti yetu imepokea:


“Wanayanga niwaombe tuendelee kuichangia timu yetu kwa sasa ili tuwape hamasa kuelekea kuua mnyama jumapili, ukishachangia klabu yako waambie na wengine wawili zaidi wachangie pia.”


Klabu ya Yanga ilianzisha utaratibu wa kuchangia timu yao kwa lengo la kutunisha mfuko wake, jambo hili limepokelewa kwa mwitikio mzuri na wapenzi na wanachama wa klabu hii.

Yanga inasemekana kuwa na mashabiki wengi sana nje na ndani ya Tanzania, Siku ya Jumapili itakutana na watani zake Klabu ya Simba Sc, katika mchezo wa Ligi kuu, Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo.

 

Sambaza....