Bocco
Blog

Bocco: Njooni kesho mashabiki mtafurahi.

Sambaza....

Nahodha wa klabu ya Simba John Bocco amewaita mashabiki wa klabu yake ya Simba na kuwaahidi furaha katika mchezo wao utakaopigwa kesho wakiwa wageni wa Yanga katika dimba la Taifa “Kwa Mkapa,”.

John Bocco ameongea hayo leo katika kikao cha kuongelea mchezo wa kesho huku akiwa sambamba na wake Sven Van Debroek pamoja na kocha wa Yanga Luc Aymael na nahodha wake Juma Abdul.

John Raphael Bocco.

John Bocco ” Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho tupo tayari. Tutacheza kwa kujituma ili tuweze kuwafurahisha mashabiki wetu  na kuweza kupata alama zote tatu.”

Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza uliisha kwa sare ya mabao mawili kwa mawili baada ta Yanga kufuta uongozi wa mabao mawili ya Simba ndani ya dakika 5 tu katika kipindi cha pili.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.