Mashindano

Yanga yatangaza mdhamini mpya!

Sambaza....

Klabu ya Yanga katika mkutano na waandishi wa habari leo wamezindua wiki ya Wananchi wakielezea ratiba nzima ya shughuli zao lakini pia wakimtangaza mdhamini mpya kuelekea siku ya Wananchi. Ambapo msimu huu itatambulika kama “Byuti Byuti”

Katika mkutano huo Makamo wa rais wa Yanga Arafat Hajji amewatambulusha CRDB Bank kama wadhamini wenza kuelekea katika wiki ya wananchi na kilele chake August nane mwaka huu.

Farid Seif (kushoto) mkuu wa kitengo cha kadi CRDB Bank pamoja na Arafat Haji (kulia) Makamo mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

“Tutakua na wenzetu wa CRDB katika Wiki hii yote ya Wananchi na siku ya Alhamis Wanayanga tuwahi mapema saa 11 ili twende kuwachukua wageni wetu CRDB halafu twende naoo klabuni naamini watazoeaa Jangwani” Arafat Hajji

Pia wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga Sportpesa wao watachangia katika zoezi la kuchangia damu wakishirikiana na hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambalo litafanyika klabuni na wachangiaji watapata jezi za Yanga bure kabisa.

Sabrina Msuya meneja mahusiano wa Sportpesa.

Yanga pia imetambulisha  wasanii watakaokuwepo katika Wiki ya Wanachi ambao ni pamoja na Chid Benz, Msaga Sumu, Mzee wa bwax, Mimi Mars, Madee, Mr Blue na Marioo

Viingilio katika siku hiyi vitakua ni 10,000 (mzinguko),  VIP C (20,000) VIP B (30,000). Halafu kutakua na VIP A 150,000  na VVIP 300,000.

Sambaza....