Tetesi

Dickson Ambundo akaribia kutua Yanga

Sambaza....

Baada ya Yanga kumsajili Wazir Junior kutoka Mbao FC ili kuimarisha eneo la ushambuliaji ndani ya timu hiyo , kuna taarifa za ndani zinadai kuwa Yanga wamehamia kwa Dickson Ambundo.

Mchezaji huyo ambaye hucheza kama winga wa pembeni ameonekana kufikia makubaliano ya kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania.

Ikumbukwe Dickson Ambundo ashawahi kucheza ligi kuu Tanzania bara akiwa na klabu ya Alliance FC baada ya hapo alihamia kwenye klabu ya Gormahia FC ya nchini Kenya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.