Ligi Kuu

Ditram Nchimbi: Nitafunga sana “hatrick”

Sambaza....

Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa Ditram Nchimbi ametoa ya moyoni leo baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya Galacha wa mabao na tovuti pendwa ya Kandanda.co.tz iliyodhaminiwa na Mgahawa Cafe and Restaurant.

Nchimbi ameiambia tovuti ataendelea kusaka mabao kadri ya nguvu za Mungu zitakavyomruhusu kuweza kufanya vyema na kutupia magoli. Huku pia akiahidi kuendelea kufunga “Hatrick” katika VPL.

Ditram Nchimbi  “Inshallah naamini nitafunga sana na sana msimu huu ili kuweza kusiadia klabu yangu ya Yanga.  Kwa uwezo wake Mungu na baraka zake, jitihada na maarifa nitapambana zifike hata 5 msimu huu. Cha muhimu na dua tuu na juhudi.”

Ditram Nchimbi “Duma” akiwa mazoezini na klabu yake ya Yanga.

Nchimbi pia alihudhuria katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo  cha Sheria na hivyo kuzima uvumi kwamba alikua anaelekea nchini Misri kwenda kufanya majaribio.

Feisal Salum na Ditram Nchimbi wamekua wakitajwa kuelekea nchini Misri kwenda kutafuta nafasi ya kucheza mpira wa kulipwa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.