Ligi Kuu

Etienne kuiongoza Azam Fc msimu ujao

Sambaza....

Kama tulivyoripoti hapo awali kuhusu safari ya Etienne Ndayiragije kutoka KMC kwenda Azam Fc, hatimaye leo imetimia.

Kocha huyo aliyewahi kufanya vizuri na Vital’o ya Burundi, na pia kuiwezesha KMC kumaliza nafasi ya nne na kupata nafasi ya kucheza Shirikisho Adrika msimu ujao, amesaini Mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu ya Azam Fc.

Hivyo, Etienne atakuwa na Azam katika michuano ya ndani na nje ya nchi msimu ujao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x