Luc Eymael, Kocha wa Yanga sc
Blog

FIFA kumfungia Luc Eymael ?

Sambaza....

Baada ya maneno machafu ambayo yalionekana kuwaudhi wapenzi wengi wa mpira hapa nchini kutoka kwa Luc Eymael , mambo yameanza kuonekana kuwa magumu kwake kutokana na kuanza kupitia changamoto mbalimbali.

Yanga wamemfuta kazi mpaka sasa hivi. Jana pia shirikisho la mpira Afrika Kusini limemfungia kufundisha  mpira katika nchi ya Attila Kusini kutokana na lugha ambazo alizitoa wakati akiwa Tanzania.

Shirikisho hilo pia la soka Afrika Kusini katika taarifa yao wamedai kuwa watapeleka ombi maalumu kwa shirikisho la mpira duniani (FIFA) na lile shirikisho la mpira barani Afrika (CAF) ili Luc Eymael afungiwe.

Sambaza....