Blog

Full ratiba ya ‘SportPesa Simba Week’ hii hapa..

Sambaza kwa marafiki....

Simba week rasmi imeanza tarehe 31-7-2019 ambapo kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kimewasili nchini kutokea nchini Afrika ya Kusini, kwa shirikia la ndege la Air Tanzania.

31-7-2019- kusaini mkataba wa miaka miwili na mdhamini wa Jezi na Vifaa vya mazoezi.

1-8-2019- Kuzindua jezi mpya ya msimu 2019/2020 ( za Nyumbani, Ugenini na Neutral ). Tukio hili litafanyika kupitia mitandao ya kijamii ya Simba na SportPesa, kuanzia saa sita usiku.

 • Uuzaji wa jezi mpya nchi nzima kuanza, klabu itatangaza ni wapi jezi hizo zitapatikana.
 • Kutakuwa na Mkutano na waandishi wa habari, kuzindua kadi Mpya za benki (Smart Card) za wanachama na Mashabiki wa Simba. (Eneo- Serena Hotel, saa tano)
 • Kuanza uuzaji wa tiketi za Platinum na Platinum Plus kwa ajili ya mechi ya Simba day dhidi ya Dynamos.

3-8-2019- Kampuni ya SportPesa kwa ushirikiano na klabu watawatembelea na kuwatia moyo watoto waishio katika mazingira magumu.

 • Wachezaji wa Simba kwenda kutoa misaada katika hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. Rai imetolewa kwa wanachama na mashabiki wote wa Simba kutembelea hospitali zilizopo karibu yao kutoa misaada kwa watu wasio na uwezo.
 • Kuchangia damu.
 • Kuzindua wimbo maalumu wa Simba. Lengo ni kuongeza hamasa kwa familia ya WanaSimba.

4-8-2019- kwa watakao nunua tiketi za Platinum na Platinum Plus watapata fursa ya kupiga picha na wachezaji wa Simba wakiwa wamevalia jezi rasmi za mechi (Photo Shoot with Simba Stars). Eneo- Serena Hotel.

 • Hamasa kubwa imetolewa kwa watoto lengo ni kukuza kizazi kipya cha kuipenda  Simba.
 • Wachezaji kutembelea vituo mbalimbali vya Watoto Yatima (Orphanage Visit) na kutoa misaada na motisha.
 • Kuipokea timu ya Power Dynamos kutoka Kwite Zambia.

5-8-2019- Matukio yanayohusiana na maandalizi ya mwisho ya mechi, ikiwemo “Pre-match meeting, Mkutano na Waandishi wa habari kwa makocha na manahodha wa timu zote mbili, Simba kufanya mazoezi taifa na kisha kuwapisha wageni wao Power Dynamos.

 • Simba Queens wakiambatana na watu wengine maarufu ambao ni mashabiki wa Simba kuitembelea  timu ya Wasichana wa Sekondari ya Makongo, kutoa hamasa, kufanya mazoezi pamoja na semina.

6-8-2019- Hii ndio siku ya kilele, Siku ya Simba day. Wito umetolewa kwa mashabiki wote kutokea kisimbasimba, kwa kununua jezi mpya au kuvaa za zamani. Mechi inatarajiwa kuanza saa 5:30 za jioni.

 • Kutakuwa na burudani uwanja wa taifa kuanzia saa tano za asubuhi.
 • Kutakuwa na mechi kabla 2 ya mechi ya saa 11 za jioni, Simba Queens saa nane za mchana Kisha  Simba U20 vs Fountain Academy.
 • Kutambulisha wachezaji na mechi kuanza.

7-8-2019- Chakula cha usiku cha pamoja (Klabu ya Simba  na Klabu ya Power Dynamos) na kisha kuwaaga wageni na kuwashukuru wadhamini wote waliofanikisha tukio la SportPesa Simba Week 2019.

KAULI MBIU. IGA UFE, THIS IS NEXT LEVEL #10YRS ANNIVERSARY OF SIMBA WEEK.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.