Blog

Gadiel Michael anaweza kucheza TP Mazembe -Mwinyi Zahera

Sambaza....

 

Jana Mwinyi Zahera alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Global Online TV . Mahojiano ambayo yaliibua masuala mbalimbali , moja ya kitu ambacho kiliibuka ni suala is Gadiel Michael na Ibrahim Ajib.

Alipoulizwa kuhusu Ibrahim Ajib na Gadiel Michael kutopata nafasi kwenye kikosi cha Simba ukilinganisha na nafasi ambazo walikuwa wanapata Yanga Chini yake alisema kuwa kila mwalimu ana falsafa yake .

Zahera

“Kila mwalimu ana falsafa , Mimi nilikuwa na falsafa yangu ambayo nilikuwa naona hawa wachezaji wanafaa kucheza Yanga . Isikute mwalimu wa Simba ana falsafa yake ambayo anaiona kuwa hawa wachezaji hawawezi kupata nafasi mara nyingi .

“Kaona eneo wanalocheza kuna watu wengine wazuri ambao wanaweza wakacheza vizuri kuliko wao ndiyo maana hawapati nafasi mara kwa mara

” Kila kocha ana falsafa yake , Leo Gadiel Michael hapewi nafasi kubwa Yanga Lakini Gadiel huyu huyu anaweza kupata nafasi kubwa timu nyingine hata TP-Mazembe ” alimalizia kocha huyo kutoka Congo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.