Zahera Yanga
Tetesi

Gwambina FC kumleta Mwinyi Zahera

Sambaza....

Timu ya Gwambina FC iliyopanda ligi kuu msimu huu inaendelea kujiimarisha kuelekea katika msimu mpya kwa kufanya sajili mbalimbali kwenye kikosi chao.

Kuna taarifa ambazo zinadai kuwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera anatazamiwa kurudi nchini kuifundisha timu hiyo ya Misungwi , Mwanza.

Kocha huyo ambaye alidumu na Yanga kwa muda wa mwaka mmoja inasemekana ameanza mazungumzo na klabu hiyo ya Gwambina FC kwa ajili ya kuja kuinoa klabu hiyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.