Moja ya mikutano ambavyo timu inaweza kutangaza viingilio au utaratibu wa mapato yao. Pichani ni Haji Manara, Msemaji wa Simba SC.
Blog

Haji Manara: Yanga walikuja kupigana uwanjani.

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba sc Haji Manara ametoa ya moyoni leo sababu ya Simba kupoteza dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara March 8 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Manara alizungumzia mchezo ule na kukiri kua walizidiwa na Yanga na walistahili kupata ushindi katika mchezo ule huku pia akisema Yanga iliwasaidia sana kuingia kwenye mechi kama “underdog”.

Japhary Mohamed akiondoa hatari mbele ya Chama na Kagere.

Haji Manara “Siku ile Yanga waliingia uwanjani kwenda kupigana na Simba hakika “fighting spirit” yao ilikua kubwa siku ile ya mchezo. Ukiangalia siku ile wachezaji wa Yanga mmoja mmoja walijitolea sanaa. Waliingia kucheza kwa nguvu maana waliamini wao ni “underdog” katika mchezo ule na ndicho kilichowaponya siku

Ukimuangalia Papy, Japahary “was fantastic” siku ile hata huyo Morisson alicheza kidogo tu lakini alifunga goli, mwisho wa siku wote walicheza vizuri lakini kipa wao Menata Mchata alikua mchezaji bora wa mechi. Sasa mchezaji bora wa mechi akiwa kipa nadhani unaojua kipi kilitokea. Huenda ingekua nane moja au saba moja kama sio michomo aliyoiokoa Menata siku ile.”

Menata Mchata!

Manara pia hakusita kuwakubali na kuwasifia wachezaji wa Yanga kwa jinsi walivyocheza katika mchezo ule dhidi ya Simba na kuweza kupata matokeo.

Haji Manara amezungumza hayo akiwa katika kipindi cha michezo cha Kipyenga cha East Africa redio.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.