David Molinga "Falcao"
Ligi Kuu

Hakuna wa kuniweka benchi -Molinga

Sambaza....

Mshambuliaji wa Yanga, David Molinga, alitabiriwa na kocha wake wa zamani Mwinyi Zahera kuwa ni lazima afunge mabao 15 msimu huu na asipofanya hivyo, basi yuko tayari kukatwa mkono ama kulipa faini ya Sh 2 milioni, kwa sasa anajifua mara mbili kwa siku ili kupunguza na kuweka mwili fiti tena akiwa na mwalimu ambaye anamsimamia.

“Jioni huwa nakwenda fukwe za bahari kwenye mchanga mwingi, hapo nafanya mazoezi ya kupunguza uzito ili kuwa mwepesi zaidi.

Nina imani kwa ratiba hii nitaonyesha tofauti kubwa na hata kuongeza idadi yangu ya mabao kutoka nane mpaka 15,” David Molinga.

David Molinga akipambana na Abdalah Mfuko wa KMC

“Kwa maana hiyo mashabiki wetu wa Yanga watulie nina imani nitafanya vitu vizuri mara baada ya ligi kurejea na wenyewe kufurahi,” aliongeza Molinga.

Kuhusu kiwango chake; “Kwa kile ambacho nimekionyesha msimu huu najiona nina nafasi kubwa ya kuwepo hapa, lakini pia nina ofa kutoka katika timu tatu tofauti.

“Kama nitasalia hapa msimu ujao Yanga, hao washambuliaji wanaohusishwa nawakaribisha kwani ushindani ambao tutauonesha mazoezini nina imani nitapata nafasi ya kuendelea kucheza mbele yao,” alisema Molinga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.