Ligi Kuu

Hata bila Morrison Yanga itashinda

Sambaza....

Bernard Morrison, shujaa mkubwa wa mechi ya watani wa jana , Simba Sc na Yanga SC ambapo alifunga gol 1 ambalo liliwapa ushindi Yanga SC kwenye mechi yao ya mwisho kuzikutanisha hizi timu zote mbili.

Bernard Morrison mpaka sasa hajaungana na kikosi cha Yanga SC ambacho kipo jijini Dodoma kwa sasa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Bernard Morrison pia hakuungana na timu yake pia mjini Shinyanga kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC . Hii ilileta hali ya sintofahamu kwa mashabiki wa Yanga SC hasa baada ya taarifa ya Bernard Morrison kuripotiwa kutakiwa Simba SC.

Kukosekana kwa Bernard Morrison kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania inaonesha kutakuwa na pengo kwenye timu ya Yanga SC , lakini Afisa Mhamasishaji wa Yanga SC amedai kuwa hakuna pengo la Bernard Morrison.

“Hakuna pengo, kina Balama Mapinduzi watacheza eneo lake na hakuna pengo lake ambalo linaonekana. Ndiyo maana tunasema Yanga SC , mwanzo mbele , mwisho mwiko kwa hiyo kuna wachezaji watacheza eneo lake” alimalizia Antonio Nugaz.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.