Sambaza....

“Usiku wa deni haukawii kuisha” hivi ndivyo kocha wa Manchester United  Jose Mourinho alivyokuwaakisubilia hatma yake katika klabu hiyo ya mashetani wekundu baada ya matokeo mabovu katika ligi na klabu bingwa barani ulaya. Hatimaye imethibitishwa kuwa kocha wa mabingwa wa Europa msimu wa 2016/17 ametimuliwa rasmi.

Takriban ni miaka mitatu tangu atimuliwe pale darajani, Chelsea tarehe 17 desemba, 2015, na leo tena anatimuliwa ikiwa ni desemba 18 na kushindwa kuifikia sikukuu ya Krismas. Katika kitu kisicho cha kawaida, Mwaka 2015 akiwa Chelsea alifukuzwa baada ya kufungwa na wanaongoza  ligi kipindi hicho walikuwa ni Leicester City na hata leo anafukuzwa baada ya kufungwa na wanaoongoza ligi kwa sasa,majogoo wa jiji Liverpool.

Kupitia ukurasa wa Twitter, klabu ya Man U imemtakia kocha huyo mafanikio mema katika kazi yake hiyo akipata timu ya kuifundisha . Hii inamaanisha kuwa, Man U na Mourinho wamemalizana vizuri.

Taarifa katika ukurasa wa ManUtd

Mourinho ameiacha klabu hiyo ikiwa katika nafsi ya 6, ikicheza mechi 17 na kujikusanyia alama 26 pekee tofauti ya alama 19 na anayeongoza ligi Liverpool akiwa na alama 45. Man U ya msimu huu chini yaMourinho imepata ushindi katika mechi 7, imefungwa 5 na kutoka sare 5 katika michezo 17 ya ligi.

Msimu huu, Mourinho ameiwezesha  Man U kufika hatua ya mtoano katika michuano ya klabu bingwa ualaya. Man Uinatarajia kukutana na mabingwa na vinara wa ligi ya Ufaransa Paris- SaintGerman (PSG) ili kufuzu raundi hii na kuiingia robo fainali ya michuano hiyo.

Mourinho ambaye aliridhi mikoba ya Luis Van Gaal  ya kuinoa Man U mwaka 2016 ukiwa ni mwaka wake wa 20 katika ligi kuu nchini  Uingereza, aliiwezesha man U kushinda ngao ya jamii, baada ya kuichapa 3-2 Southamptom,  shukrani zikimuendea ZlatanIbrahimovic. Katika msimu huo, Man u ilimaliza ligi ikiwa katika nafasi ya 6,lakini ilifuzu kucheza mashindano ya Klabu bingwa ulaya baada ya kuilaza Ajax  2-0 katika fainali za kombe la Europa kisha Man U kufuzu katika msimu wa mwaka 2017/18.

Msimu wa pili wa Mourinho akiwa na man U haukuwa msimu mzuri, kwani hakubeba kikombe chochote, akiishia kushika nafasi ya pili,katika msimamo wa ligi kuu England, akitolewa katika hatua ya 16 bora dhidi ya Sevilla katika michuano ya klabu bingwa  barani ulaya na kisha kufungwa na Chelsea katika fainali ya kombe la FA.

Kutimuliwa kwake hakujawashangaza wengi kwani,yalikuwa ni matarajio ya mashabiki wa Man u . Katika kipindi chote hicho Mourinho amekuwa katika hali ya kutoelewana na wachezaji akiwemo Paul Pogba nakusababisha klabu kukosa muunganiko ndani na hata nje ya uwanja.

Ripoti zinadai kuwa, Kocha msaidizi   Michael Carrick hatopewa jukumu la moja kwa moja la kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, hadi pale kocha mkuu atakapotangazwa  katika majira ya  kiangazi.

Carrick (kushoto) wakati wa mechi dhidi ya Liverpool.

Zinedine Zidane na Maurizio Pochettino ndio  wanaopigiwa chepuo zaidi ya kurithi mikoba ya mreno huyo pale Old Traford.

Sambaza....