Mukoko Tonombe
Ligi Kuu

Hii ndio maana ya kikosi kipana!

Sambaza....

Kikosi cha Yanga mpaka sasa kimecheza mchezo mmoja tu mbele ya mashabiki wao wa Yanga dhidi ya Aigle Noir katika uwanja wa Mkapa katika kilele cha siku ya Wananchi.

Mchezo huo mmoja umetosha kuonyesha upana wa kikosi walichonachi Yanga kuanzia kwa walinzi mpaka washambuliaji. Yanga hii sio ya msimu uliopita iliyoanza kwa kusasua katika michezo yake ya mwanzo.

Kikosi cha Yanga cha msimu 2019/2020

Yanga imesajili wachezaji wapya 14 huku ikigusa kila eneo, kwa maana kuanzia eneo la ulinzi, kiungo na ushambuliaji. Sehemu ya walinda mlango pekee ndio hakuna ingizo jipya.

Karibu kila sehemu ina wachezaji wawili au watatu wenye viwango sawa ama vinakaribiana uwanjani.

Tazama kikosi cha Yanga kilivyosheheni!

  1. Metacha, Shikalo, Kabwili
  2. Kibwana Shomari/ Paul Boxer
  3. Yassin Mustapha/ Adeyum Saleh
  4. Abdallah Ninja/ Makapu
  5. Lamine Moro/ Mwamunyeto
  6. Mukoko/ Makame/ Mauya
  7. Kaseke/ Mahadhi/ Mapinduzi
  8. Feisal/ Niyonzima/ Carlinhos
  9. Waziri Junior/ Sarpong
  10. Nchimbi/ Yacoube
  11. Kisinda/ Farid Mussa/ Mahadhi.
Farid Mussa

Kwa kikosi hiki unaona kabisa kazi kubwa inabaki kwa mwalimu Zlatiko na msaidizi wake Mwambusi kuandaa na kutengeneza muunganiko wa wachezaji ili kuleta tija uwanjani.

Kitu pekee wanachotakiwa kuwa nacho wapenzi wa Yanga ni uvumilivu katika kipindi ambacho mwalimu anaanda timu kwa maana muunganiko wa timu unahitaji muda. Hivyo hata matokeo yasipokua mazuri katika mechi za mwanzo wasianze kutafuta mchawi wala kulaumiana.

Sambaza....