Sambaza....

Klabu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imeridhia kuvunja mkataba na kiungo mkongwe Humoud Abdulharim Ali baada ya kuridhika kuwa amekuwa mtovu wa nidhamu kwa kuwatongoza wake na wachumba wa wachezaji wenzake.

Akizungumza na mtandao huu katibu msaidizi wa KMC Walter Urio amesema walipata malalamiko kutoka kwa mchezaji anayelala chumba kimoja na Humoud kuwa amekuwa na tabia ya kumtongoza mchumba wake kitendo ambacho ni kinyume na maadili.

Aidha mbali na hilo pia Walter amesema walipata malalamiko kutoka kwa mchezaji ambaye si wa klabu ya KMC kuwa Humoud amekuwa akimtongoza mke wake jambo ambalo limezidi kuichafua taswira ya klabu yao.

Humud

“Humoud ana mchezaji anayeishi naye chumba kimoja, sasa yeye akaenda akaiba namba ya mchumba wa mtu kwenye simu akijua kuwa anamahusiano, akaanza kumshawishi aachane naye na aje kwake, hilo lilileta mtafaruku mkubwa,”

“Hakukifanya kwa mtu mmoja amefanya kwa mchezaji mwingine pia, alitupigia simu uongozi, tena huyo ni mke na ushahid akatuletea, akatuambia kuna mchezaji wenu anamsumbua mke wangu na sio mara moja, na nishamueleza akaniambia ataacha lakini bado ameendelea.” Walter amesema.

Humoud ambaye amekuwa na KMC toka ligi daraja la kwanza ameachwa kutokana na tabia hiyo ambayo inaelezwa kuwa ni kama kawaida yake toka akiwa katika vilabu vingine kama Azam.

Mbali na hilo pia Humoud ametajwa kugomea michezo kadhaa kutokana na kuwekwa benchi kama ule ambao KMC walicheza na Coastal Union akidai kuwa amesahau vifaa vyake jijini Dar es Salaam jambo ambalo Walter amelitaja kurudisha nyuma mipango ya klabu ambayo wamejiwekea.

Walter amesema Humoud atapaswa kuilipa klabu hiyo fidia ya gharama ambazo wamemuhudimia kwani mbali na makosa hayo yeye ndiye aliyepeleka barua ya kutaka kuachana na klabu hiyo na wao kumkubalia kutoka na kuwa na nidhamu mbovu.

Sambaza....