Ibrahim Ajib Migomba.
Tetesi

Ibrahim Ajib huku, Never Tigere Msimbazi!!

Sambaza....

Dirisha la usajili likiwa limefunguliwa tangu tarehe moja mwezi huu baadhi ya vikosi vya Ligi Kuu Bara tayari vimeshaanza kujiimarisha kuelekea msimu ujao kwa kuanza kusajili wachezaji.

Kiungo Ibrahim Ajib aliekosa nafasi katika klabu ya Simba baada ya kurejea akitokea Yanga huenda akatolewa katika timu baada kushindwa kugombea nafasi mbele ya kina Chama, Luis, Kahata na Dilunga.

Never Tigere

Tetesi zilizopo ni kwamba Simba na Azam fc zinaweza kufanya mabadilishano ya wachezaji wao wa maeneo ya kiungo mshambuliaji ambapo Ibrahim Ajib atakwenda Azam fc huku Never Tigere akatimkia Simba sc.

Azam fc wakiwa tayari wameshasajili viungo watatu Ally Niyonzima, Awesu Awesu na Ayoub Lyanga. Lakini kwa upande wa Simba bado mpaka sasa hawajafanya sajili yoyote kuelekea msimu ujao.

Sambaza....