Sambaza....

Timu ya soka inayomilikiwa na jeshi la Kujenga Taifa JKT Tanzania imeendeleza kugawa vipigo katika michezo inayopigwa katika uwanja wao wa nyumbani baada ya leo kuiadhibu African Lyon ya Dar es salaam.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Generali Isamunyo bao lá Abdulrahmani Mussa katika dakika ya 50  lilitoshakuwapa alama tatu vijana wa Bakari Shime  waliokua wenyeji.

Lyon ikiongozwa na washambuliaji wao Victor da Costa na Haruna Moshi “Boban” hawakuweza kabisa kufurukuta mbele ya walinzi wa JKT Tanzania wakiongozwa na Mohamed Fakhi na Maiko Aidan.

JKT Tanzania sasa wanasubiri kuwakaribisha Allience fc katika dimba lao la nyumbani mchezo utakaopigwa Jumamosi hii tarehe 6 October!

Sambaza....