Sambaza....

Mshambuliaji na nahodha wa Simba John Raphael Bocco amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya ufungaji katika Ligi Kuu Bara katika msimu huu.

John Bocco anakua mchezaji wa kwanza kuweza kufunga magoli 100 katika Ligi Kuu ya Tanzânia Bara tangu ilipobadilishwa jina kutoka Ligi daraja lá kwanza Tanzania na kuitwa Ligi Kuu Bara. Ameweza kufikisha mabao hayo baada ya kuweza kuwafunga Mwadui FC mabao mawili katika mchezo wa leo  wa ligi kuu Bara.

John Bocco ameweza kufunga magoli hayo akiwa ametumikia klabu mbili pekee katika Ligi. Alianza Azam fc halafu akahamia Simba na kuweza kutimiza idadi ya magoli 100.

Katika magoli hayo 100 John Bocco amefanikiwa kufunga magoli 84 akiwa na AzamFc  huku akifunga magoli 16 akiwa na Simba.

John Bocco ambae safari yake ya mpira ilianzia katika klabu ya Gonga FC ya Kijitonyama  baadae kupitia katika shule ya vipaji ya Tegeta secondary. Baada ya hapo alifanikiwa kusajiliwa na Cosmo Politan ya Kariakoo na ndipo Azam fc walipomuona na kumsajili mpaka anafanikiwa kuwapandisha katika Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2008.

K

Sambaza....