Tetesi

Jose Mourinho anarudi tena Old Trafford.

Sambaza kwa marafiki....

Tajiri mpya anayetarajiwa kutua katika klabu ya Newcastle United, Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan, amemuweka meneja wa zamani wa klabu ya Manchester United na Chelsea Fc nchini Uingereza kama meneja anayemuhitaji kwa msimu ujao.

Jose Mourinho, ambaye amekuwa mchambuzi tu wa soka tangu atemwe na klabu ya Manchester United, inasemekana pia yupo tayari kuzungumza na tajiri huyo, na tayari kitita kikubwa cha pesa kimetengwa kwaajili ya kumvuta Mourinho pale.

Jose Mourinho

Newcastle ambayo mmiliki wake wa sasa ni Mike Ashley, bado hajatoa ruhusa ya mabadiliko hayo. Lakini huenda ikawa hivyo kutokana na ushindani ulioopo katika ligi kuu ya Uingereza.

Kama atarudi EPL, hi inamaana sasa ataenda kama mgeni tena katika uwanja wake wa nyumbani zamani, Old Traford, katika klabu ya Man Utd.

Mourinho hajawahi kupata ushindi nyumbani kwa Newcastle akiwa na Chelsea na Man Utd. Katika mechi 7, kapoteza mechi nne na kutoka sare tatu. Bila shaka anatamani kurudi pale ili aone yaliyomo kama yamo.

 

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.