Khalid Aucho wa Yanga akimdhibiti Pape Sakho
ASFC

Jumamosi tulivu ya Sato na Sangara.

Sambaza....

Kama kumbukumbu zangu ziko sawia basi jumamosi hii itakuwa tarehe 28 ya mwezi May mwaka 2022. Nini kipo kwenye tarehe hii? ambayo mimi binafsi nimeiita ‘Jumamosi tulivu’.

Basi nilile pambano la kukata na shoka baina ya mahasimu wakubwa wawili nchini Tanzania wao wakitaka kuitwa ‘watani wa jadi’ na wala siyo hilo neno lenu la “mahasimu”.

Simba na Yanga wanakwenda kukutana kwa mara ya 112 tangu timu kuanzishwa kwa zaidi ya miaka 85 iliyopita, kumbukumbu zinaonesha Yanga ilianzishwa mwaka 1935 huku Simba ikiasisiwa 1936 tangu nyakati hizo wao ni wapinzani wakubwa kama si washindani wakubwa kwenye soka letu.

Meddie Kagere akipambana na Kelvin Yondani.

Hivyo basi kuelekea game yao huwa inakuwa gumzo kubwa si nchini Tanzania tu bali pande zote Duniani hususani Africa Mashariki na Kati ambayo wengi wanaufahamu utamaduni wa “derby” hii.

CCM Kirumba patakuwa patamu siku hiyo, najua mashabiki wa soka wanaona kama muda hauendi ili kukata ‘mzizi wa fitna’ kwenye mechi isiyo ya ligi mechi ya kikombe ambayo ipo kwenye mfumo wa mtoano, hivyo ni lazima mshindi apatikane kama ni ndani ya dakika 90 au kwenye changamoto ya mikwaju ya matuta. 

Kiufundi timu zote zipo vizuri kwa asilimia kubwa cha msingi ni utayari wa wachezaji wao kwenye kupambania jezi yao japo eneo hili litatokana na ujenzi wa kisaikolojia
toka kwenye mabenchi yao ya ufundi.

Kama ilivyo katika mchezo huu kuna sehemu zenye ushindani mkubwa zaidi ‘ key battle’ basi eneo la kwanza ni Mayele vs Inonga.

“Battle” hili kwa sasa ndiyo gumzo ndani ya derby ya kariakoo kuliko maeneo yote kwa mchezaji mojamoja zaidi ya hapo ni ya “team combination.”

Fiston Mayelle vs Inonga Baka.

Makocha wote wawili ni waumini wa mifumo yenye idadi kubwa ya viungo pale kati ili kuleta usawa mzuri kwenye kushambulia na kijihami.

Nabi katika 4-2- 3-1 ambaye mara nyingi huanza na Djigui Diarra, Djuma Shaban, Shomari Kibwana, Dickson Job, Bakar Mwamnyeto, Yannick Bangala, Zawadi Mauya
Sure Boy, Fiston Mayele, Feisal na Farid Mussa.

Pablo huwatumia Manula, Kapombe, Tshabalala, Onyango, Wawa, Inonga, Kanoute Mzamiru, Bocco, Kibu  na Sakho.

Mlinzi wa kulia wa Simba Shomary Kapombe akimthibiti Kibwana Shomary wa Yanga.

Kama uteuzi wa vikosi vitakuwa hivyo kwa asilimia kubwa uwezo binafsi wa mchezaji ndiyo utaamua game na si muunganiko wa timu kwa sababu mpangilio huo nani aina ya wachezaji itasababisha ‘intact game ‘ kutokuwa na mianya hivyo suluhisho ni uwezo mkubwa wa kupiga vyenga ili kupunguza na kulazimisha kupata nafasi zaidi au kupiga mashuti ya mbali(ambayo tunaiterms ni uwezo binafsi).

Tukumbushwe kuwa mechi haina sare ni lazima mshindi apatikane hivyo dakika 90 isipotoa majibu matuta yatatoa majibu
na lazima makocha wazifanyie kazi kwa kina.

Kila Lakheri Watani….


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.