Kagere akiwa ameshika kiatu chake MK4 baada ya kukabidhiwa na Kandanda
Blog

Kina Morrison , Kagere kupimwa Corona !

Sambaza....

Ligi kuu Tanzania bara mpaka sasa hivi iko njiani kurudi tena. Wakati tunasubiri wakati sahihi wa kurudi ligi hii na namna ambavyo itachezwa iwe kwenye kituo kimoja au kama kawaida kwa mechi za nyumbani.

Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara kupitia kwenye mwenyekiti wake Steven Mguto wamedai kuwa mpaka sasa hivi wamepanga kila mchezaji kupimwa Corona kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara.

Niyonzima

“Tumewasiliana na idara yetu ya afya , na tumetoa baadhi ya mapendekezo kwa serikali namna ya kulinda afya za wachezaji kipindi ambapo ligi kuu Tanzania bara itakaporejea”.

“Kuhakikisha ulinzi wa afya za wachezaji , tutahakikisha wachezaji wote wanapimwa ugonjwa wa Corona kabla ya ligi kuanza, pia viongozi wa vilabu na makocha watapimwa”- alimalizia Steven Mguto , mwenyekiti wa bodi ya ligi.

Clatous Chama

Baada ya tamko hilo , Haji Manara amedai kuwa timu yake ya Simba SC imelipokea kwa mikono miwili tamko hilo la mwenyekiti wa bodi ya ligi na watalifanyia kazi ipasavyo.

“Kupima afya ni jambo jema , watu wengi wanaona mtu kukutwa na ugonjwa wa Corona ni kitu cha ajabu . Corona inaweza ikampata mtu yoyote katika mazingira yoyote” alisema Afisa habari huyo wa Simba.

“Sisi tutawapima wachezaji wetu watakaporejea kazini , hakuna shida tumelipokea kwa mikono miwili kabisa agizo hilo la bodi ya ligi”- alimalizia Afisa habari huyo wa Simba SC.

Naye daktari wa Yanga SC , Doctor Ngazija amedai kuwa klabu hiyo itazingatia kila kitu kwa ajili ya kujikinga na Corona kwa kulinda afya za wachezaji .

“Tunashauriwa kuvaa masks , mipira yetu tutaipulizia dawa na wachezaji wataruhusiwa kutumia kiatu kimoja tu baada ya mazoezi , hicho kiatu hawatoruhusiwa kuingia nacho kwenye chumba cha kubadilishia nguo”- alisema doctor Ngazinja .

“Klabu itawapa wachezaji viatu vya ziada na kuhusu suala la kupimwa wachezaji watapimwa ugonjwa wa Corona kabla ya ligi kuanza” alimalizia doctor Ngazija

Sambaza....