Shirikisho Afrika

Kiongozi Simba: Pablo haendi popote, tuna ofa kibao za wachezaji wetu

Sambaza....

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema wao kama Simba hawajatoa taarifa yoyote kuhusu kumfukuza kocha kazi. Simba imetolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na hivyo kushindwa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu yakufika nusu fainali ya michuano hiyo.

“Mpaka sasa Simba haijawahi kutoa taarifa zozote kuhusu kocha, sisi Simba bado tunamashindano yapo mbele yetu na tunataka kufanya vyema.” Murtaza Mangungu

“Hizi taarifa za kocha sijui mmezitoa wapi. Hakuna taarifa yoyote ya klabu iliyosema kuhusu kumfukuza kocha.” Alisema Mangungu.

Pablo Franco

“Ni kweli Simba ina target yake, labda kama kuna wenzentu wengine ambao wanakwenda tuu bila malengo kwamba lolote litakalotokea ni sawa tuu. Kocha wetu bado ana mkataba nasisi na bado tuna mechi mbele yetu hivyo sitegemei tena kuulizwa  kuhusu huu uzushi wa kumfukuza kocha (Pablo Franco).” Mwenyekiti aliongeza.

Murtaza Mangungu pia alisema kutokana na ubora wa wachezaji wao waliouonyesha katika michuano hiyo wamepata ofa kibao za wachezaji wao kutakiwa na vilabu vingine.

Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani katika moja ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kwakweli kutokana na ukubwa wa klabu ya Simba wachezaji wanapata ofa mbalimbali katika nchi mbalimbali za Afrika na hii ni kutokana na kiwango  wanachoonyesha katika michuano hii.” Murtaza Mangungu.


Sambaza....