Ligi Kuu

KMC kamili kuivaa Stand United ugenini.

Sambaza kwa marafiki....

Wana “KinoBoys” watoto wa Manispaa ya Kinondoni KMC tayari wapo jijini Shinyanga kuwakabili wapinzani wao Stand United katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa kamili ya Klabu hiyo imeeleza ni jinsi gani imejiandaa na ushindani katika mchezo huku pia ikiwakosa baadhi ya nyota wake muhimu kutokana na majeruhi.

“Kikosi kimefika salama Shinyanga na leo asubuhi timu imefanya mazoezi katika dimba la Kambarage tayari kabisa kwa mchezo wa kwanza wa ugenini katika raundi ya pili. Mwenyeji wetu ni Stand United hivyo tupo tayari kwa ushindani.” Imeeleza taarifa rasmi ya klabu.

“Tutawakosa James Msuva, Sixtus Sabilo na Rayman Mgungila walio majeruhi ambao tumewaacha Dar es salaam kwaajili ya matibabu zaidi. Matokeo mazuri ya timu zote mbili kwa kiasi kikubwa yatachangia mchezo mzuri, Kmc imetoka kumfunga Coastal 5 kwa mbili huku  Stand United wao wakimpiga Yanga sc bao moja kwa sifuri.”

Stand united inategemewa kuikaribisha KMC katika dimba la Kambarage kesho Ijumaa saa kumi jioni.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.